Madee atoa habari njema kwa mashabiki wa Dogo Janja
Madee ana habari njema kwa mashabiki wa Dogo Janja.
Awali kulikuwa na taarifa kuwa Tip Top itaachia wimbo waliomshirikisha Diamond lakini imesogezwa mbele kupisha kazi ya Dogo Janja.
Madee ameiambia Bongo5 kuwa imewabidi wamwachie Dogo Janja na wasanii wengine watoe kwanza kazi zao.
“Kama unavyojua Tip Top tulikuwa na matatizo ya kufiwa, alianza Abdu Bonge, akaja baba yake Babu Tale, sasa hivi vitu vilisababisha kusimama kutokana na mwingilino wa ratiba. [Collabo na Diamond] itatoka lakini tumeisogeza mbele na sasa hivi waanze kwanza wasanii wetu. Kwahiyo project zinazokuja ni za akina Dojo Janja na wasanii wengine,” amesema Madee.
Post a Comment