Image result for tigo banner

Mashairi ya wimbo wa Tupac ‘Ambitionz Az A Ridah’ kupigwa mnada

Ikiwa ni miaka 19 imepita toka legend wa Hip Hop, Tupac Amaru Shakur afariki dunia (Sept 13, 1996), karatasi zenye mashairi ya wimbo wake uitwao ‘Ambitionz Az A Ridah’ zinatarajiwa kupigwa mnada baadae mwezi huu huko jijini London.
Tupac
Kwa mujibu wa New York Daily News, karatasi mbili zenye mashairi hayo aliyoandika kwa mkono mwaka 1995 alipokuwa jela, zitapigwa mnada na Sotheby’s Auction ya Uingereza kwa kiasi cha kati ya $47,000 hadi $78,000 (sh milioni 101 na m169 ) kwenye mnada utakaofanyika Septemba 29 mwaka huu.
‘Ambitionz Az A Ridah’ ni wimbo wa kwanza kwenye album ya ‘All Eyes On Me’ ya Tupac, na ndio wimbo wa kwanza aliorekodi mara baada ya kutoka jela. Ulitoka rasmi mwaka 1996

No comments

Powered by Blogger.