Timu ya taifa ya Tanzania na Nigeria September 5 zimekutana kucheza mechi ya kuwania tiketi ya kufuzu kucheza AFCON 2017, ikiwa ni zaidi ya miaka 20 toka zikutane katika mechi za mashindano. Nigeria inayonolewa na kocha mzawa Sunday Oliseh ndio imecheza mechi ya kwanza toka ianze kufundishwa na kocha huyo.
Kwa upande wa Taifa Stars ambayo haina point hata moja katika kundi lake baada ya kufungwa mchezo wa kwanza na timu ya taifa ya Misri kwa jumla ya goli 3-0, imeshuka uwanjani kuwania point 3 ili iweze kukufua matumaini ya kupata tiketi ya kucheza AFCON 2017.

William Ekong akimkaba Mbwana Samatta
Mechi iliyochezwa uwanja wa Taifa Dar Es Salaam imemalizika kwa timu zote kutoka sare ya bila kufunga, japo Taifa Stars kupitia kwa Mrisho Ngassa na Thomas Ulimwengu ilipoteza nafasi mbili za wazi.
Hizi ni picha za mechi hiyo mtu wangu.

Golikipa wa Nigeria Ikeme Onora ndiye aliyekuwa mbadala wa Vincent Enyeama

Mbwana Samatta akijaribu kumtoka beki wa Nigeria Solomon Kwambe

Mbwana Samatta katika harakati za kutafuta nafasi

Mrisho Ngassa akiwa chini baada ya kupata maumivu

Thomas Ulimwengu akijaribu kumtoka Kingsley Madu

Ikeme Onora alipokuwa mkali kwa mabeki zake baada ya shambulizi la Taifa Stars

Farid Musa akionyesha umahiri wake

Mrisho Ngassa akimkimbia Igboun Emekea

Farid Musa akiwa ameanguka chini huku William Ekong akiendelea na harakati za kuokoa

Mrisho Ngassa akitafakari namna ya kupata nafasi ya kufunga

Said Hamis Ndemla akiingia kuchukua nafasi ya Mudathir Yahaya

Mrisho Ngassa baada ya kukosa goli

Ikeme Onora akiwapanga mabeki wake

John Bocco na Mbwana Samatta

Igboun Emekea akiwa chini baada ya kupata maumivu
Madaktari na watu wa huduma ya kwanza wakitoa huduma ya kwanza kwa mchezaji wa Taifa Stars
Post a Comment