MISRI yarudi kwenye ubora wake FIFA
Misri imerejea tena katika kundi la mataifa 50 bora kwa soka duniani kwenye orodha ya Fifa ya mwezi Septemba.
Taifa hilo lilipanda hatua tatu na sasa limo nambari 49, hii ikiwa ni mara yao ya kwanza kwao kuwa katika 50 bora mwaka huu.
Mwaka
2014, walikuwa wamepanda hadi nambari 24 lakini wakaporomoka kutokana
na kushindwa kwao kufuzu kwa Kombe la Taifa Bingwa Afrika 2017.
Kwingineko, Rwanda ndiyo nchi pekee iliyopanda Zaidi ya hatua 10 duniani, baada ya kupanda hatua 13 na kutua nambari 78.
Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Congo imo nambari 59, Uganda imo nambari 74, Sudan
87, Ethiopia 99, Kenya 116, Burundi 132, Tanzania 140 na Sudan Kusini
195.
Duniani, Argentina bado inaongoza ikifuatwa na Ubelgiji, Ujerumani, Colombia na Brazil.
Mataifa
bora ya Afrika kwa mujibu wa orodha hiyo mpya ya Fifa ndiyo haya,
nambari iliyo kwenye mabano ikionyesha nambari kwa jumla duniani:
1 (19) Algeria
2 (21) Ivory Coast
3 (27) Ghana
4 (33) Tunisia
5 (38) Senegal
6 (42) Congo
7 (42) Cameroon
8 (49) Misri
9 (53) Nigeria
10 (56) Cape Verde
Post a Comment