Nay wa Mitego akana kutoka kimapenzi na msanii Pam D
Rapper Nay wa Mitego amekanusha kutoka kimapenzi na msanii wa muziki Pam D baada ya kuonekana kuwa karibu.
Nay amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio kuwa Pam D ni mshkaji wake na sio mpenzi wake kama watu wanavyosema kutokana kuwa naye karibu.
“Kuna hali ambayo ipo kwa vijana kwamba tufanye hivi na hivi lakini hatuwezi kuwa permanent ila kwangu mimi ni mshkaji wangu tu,” alisema Nay.
Post a Comment