Image result for tigo banner

Picha: Ndege ya British Airways yashika moto katika uwanja wa ndege wa Las Vegas ikiwa na abiria 159

Ndege ya shirika la ndege la Uingereza, British Airways ilishika moto ikiwa katika uwanja wa ndege wa Las Vegas, Marekani ilipokuwa ikijiandaa kwa safari ya London siku ya Jumanne, September 8.
ndege-1
Maafisa wa uwanja huo wamesema kuwa takribani watu 14 walikimbizwa hospitali wakiwa na majeraha madogo madogo.
ndege-2
Msemaji wa US Federal Aviation Administration, Ian Gregor amesema kuwa injini ya kushoto ya ndege hiyo aina ya Boeing 777-200 ilishika moto muda mfupi kabla ya kuanza kuruka na kusababisha moshi mkubwa kutanda eneo hilo. Hata hivyo moto huo ulifanikiwa kuzimwa.
ndege-3
Taarifa iliyotolewa na British Airways, imesema kuwa ndege hiyo ilipata hitilafu za kiufundi wakati ikijiandaa kuruka.
ndege-4
Abiria wakisaidiwa kutolewa kwenye ndege hiyo kupitia mlango wa nyuma
Ndege hiyo ilikuwa na abiria 159 pamoja na wafanyakazi 13.
ndege-5
Source: BBC

No comments

Powered by Blogger.