Image result for tigo banner

Diamond, Vanessa Mdee na Ommy Dimpoz washinda tuzo za Afrimma

Diamond Platnumz ameibuka na ushindi mkubwa zaidi kwenye tuzo za Afrimma zilizofanyika Dallas, Marekani alfajiri ya leo kwa saa za Afrika Mashariki.
12093277_879680755446345_1737082731_n
Diamond ameshinda jumla ya tuzo tatu ikiwemo ya msanii wa mwaka
Muimbaji huyo ameshinda tuzo tatu; Best Dance Video ya wimbo wake Nana, Best Male East Africa na Artiste Of The Year.
12105996_1219864901363470_306096200_n
Diamond amepost picha hiyo juu kwenye Instagram na kuandika: Dah, I really don’t know What to say, … dha! hata sijui nizungumze nini… (Eeh Mungu baba tunakushkuru sana kwa kuzidi kuunyanyua na kuupa Thamani mziki wetu wa Afrika Mashariki…tafadhali endelea kutushika mkono, usituache.
“EA well represented at the #Afrimma2015 & The Best Winner of the night goes to @diamondplatnumz with 3 Awards!! Salute all EA,” ameandika mtangazaji wa Citizen TV/Radio Citizen, Willy M Tuva aliyekuwepo kwenye tuzo hizo.
Pia wimbo alioshirikishwa na kundi la Bracket, Alive umeshinda tuzo ya Best Inspirational Song.
Vanessa Mdee ameshinda tuzo ya Best Female East Africa.
12145300_972400302833337_664949009_n
“Asante Asante Sana. You believed in me. Thank you,” ameandika kwenye Instagram.
10246129_438188206382165_1000817279_n
Naye Ommy Dimpoz ameshinda tuzo ya Best New Comer

No comments

Powered by Blogger.