Image result for tigo banner

Hizi ni Couple tano za wasanii zenye Nguvu zaidi Bongo

Hizi ni couple za Bongo ambazo, zina make headline mara nyingi hasa kwenye magazeti na mitandao ya kijamii.

Vanessa Mdee na Jux
Wawili hawa  waliojaa mahaba, ukiacha mapenzi pia wameonekana wakifanya kazi pamoja baada ya Vanessa kutokea kwenye video ya Jux ya Sisikii, moja ya  ngoma kali mjini. Vanessa na Jux wamekuwa wapenzi wenye mvuto sana kwa mashabiki zao hasa, kwa kile walichofanya cha kuchora tattoo za kufanana.
1vee


Diamond na Zari
Dangote aka Baba Tiffa baada ya kuachana na mrembo Wema Sepetu, alijikuta kazama kwa mtoto wa Kiganda Zarina Hassan ambae pia ni mama wa mototo wake wa kwanza wa kike Baby Tiffa, wawili hawa wameonganisha mataifa haya mawili na kuwa gumzo ndani na nje ya nchi.  Kuanzia kwenye magazeti hadi mitandao ya kijamii hasa instagram.

1dimo
Ally Kiba na Jokate
Japokuwa couple hii ni mpya lakini ni moja kati ya couple zinazo tengeneza headline Jokate ambaye alishawahi pia kutoka na Diamond, Amekuwa akionekana na kiba maeneo mbalimbali hadi nje za nchi, kama walivyonaswa wakila good times Nairobi Kenya. Mwanzo wawili hawa walikana kuwa na mahusiano lakini sasa kila kitu kinaonyesha dhahiri kuwa ni wapenzi.


Aunty Ezekiel na Mose Iyobo

Mkali wa filamu Bongo, ambae aliolewa na ndoa kubwa tu, mjini, maarufu kama mama Cookie, mtoto aliezaliwa nje ya ndoa yake, ila bila wasiwasi  ameonekana akifurahia penzi la mcheza dance huyo wa Diamond, Mose Iyobo licha ya kuwa mdogo kiumri kwake wawili hawa wameonyesha mapenzi na kuleta gumzo miongozi mwa washabiki wao.

Linah Sanga na William Bugene
William ambae inasemekana ana undugu na Zarina Hassan –Zari amekuwa akimtokea mwadada linah na inasemekana safari za Linah kwenda South Africa kwajiri ya kazi zake za kimuziki kaka willy  alisimamia show nzima. Linah alidhibitisha kuwa na furaha na willy baada ya kutoa ngoma ya No stress. Na inasemekana jamaa amesha mfikisha Linah nyumbani kwao. Tetezi hizo zitadhibitishwa baada ya kumuona lina akiwa katika wazi jeupe. William na Linah nimoja ya couple matata mjini.
1will

No comments

Powered by Blogger.