Image result for tigo banner

Joh Makini, G-Nako na Nikki Wa Pili kuachia single 3 mpya wiki Ijayo, 2 zimefanyiwa video na Justin Campos

Rappers wa Weusi wako tayari kulichafua anga la muziki kwa kuachia ngoma tatu mpya wiki Ijayo baada ya uchaguzi.
WEUSIII
Takribani miezi miwili iliyopita Joh Makini na G-Nako walienda Afrika Kusini kushoot video mbili mpya, moja ikiwa ni collabo ya Joh na rapper wa Afrika Kusini, AKA ‘Don’t Bother’ na nyingine ni single ya G-Nako iitwayo ‘Original’.
Nyimbo zote hizo mbili pamoja na nyingine ya Nikki Wa Pili iitwayo ‘Baba Swalehe’ zitatoka rasmi wiki Ijayo japo hawajasema tarehe.
weusi2
Kupitia Instagram Joh Makini pia amepost:
“Baba swalehe @nikkwapili
Original @gnakowarawara
Don’tbother feat.@akaworldwide
Produced by @nahreel #TheIndustry
Loading…….”
Nikki ameiambia Bongo 5 kuwa Nyimzo za Joh Makini na G-Nako zitaanza kutoka video, huku yake itatoka audio kwasababu bado haja shoot video. Ameongeza kuwa zitapishana siku mbili au tatu, lakini zote zitatoka wiki Ijayo.
Nyimbo zote tatu zimetayarishwa na producer wa The Industry, Nahreel

No comments

Powered by Blogger.