Naj uso kwa uso na Barnaba.
Barnaba ni mtu busy pengine kuliko wasanii wote kwa sasa.
Muimbaji huyo licha ya kuanzisha studio yake, High Table Sound, ameanzisha lebo na bendi yake pia huku akiendelea kufanya kazi aipendayo zaidi – kuandika nyimbo.
Miongoni mwa wasanii wanaotarajiwa kunufaika na kipaji chake ni muimbaji Naj ambaye miaka ya hivi karibuni alipotea. Wawili hao wameingia studio usiku wa kumkia Alhamis hii na kurekodi ngoma ya pamoja kwenye studio hizo.
“Helloooo Tanzania we out here working with the beautiful @najdattani ameandika Barnaba kwenye picha aliyoiweka Instagram.
Naye Naj amepost picha hiyo na kuandika: @ the studio @hightablesound kwa Chief @barnabaclassic now.
Naj aliwahi kuhit na wimbo Don’t Let Me Go aliomshirikisha Mr Blue. Pia aliwahi kushirikishwa na Fid Q kwenye wimbo wake Swagga Don.
Post a Comment