Rihanna atangaza jina la album yake mpya
Hatimaye Rihanna ametangaza jina album yake ya nane. Album hiyo inaitwa Anti.
Muimbaji huyo pamoja na kutaja jina la album yake, alizindua pia artwork yake usiku wa Jumatano jijini Los Angeles mbele ya umati wa watu.
Cover hiyo ni picha yake akiwa mtoto kwenye siku yake ya kwanza kwenye daycare. Ameshirikiana na mchoraji aitwaye Roy Nachum, aliyeongeza manjonjo.
Rihanna alisema album hiyo ipo tayari japo hakutangaza tarehe yake ya kutoka.
Post a Comment