Rihanna kuigiza kwenye filamu mpya ‘Valerian’
Director atakayeiongoza filamu mpya iitwayo ‘Valerian’, Luc Besson ametangaza rasmi kuwa mwimbaji maarufu Rihanna ataigiza kwenye filamu hiyo na atakuwa na nafasi kubwa.
Kupitia Instagram Luc aliandika, “RIHANNA is in VALERIAN!!!!! ….and she has a big part!! I’m Sooo excited!!!”.
Filamu hiyo ambayo itakuwa na bajeti kubwa itaanza kushootiwa mwezi January, 2016 huko Ufaransa, huku ikitarajiwa kutoka July 21, 2017.
Kwa sasa mashabiki wa Riri wanasubiri kwa hamu album yake mpya ‘ANTI’ ambayo inatarajiwa kutoka hivi karibuni.
Post a Comment