Wimbo mpya wa Vanessa Mdee ‘Never Ever’ kutoka Jumatatu ijayo
Vanessa Mdee ataachia wimbo wake mpya ‘Never Ever’ Jumatatu ijayo.
Kava la single mpya ya Vanessa Mdee ‘Never Ever.’ Picha ilipigwa na Osse Greca Sinare
Wimbo huo umetayarishwa na prodecer wake, Nahreel wa The Industry. Wimbo uliopita, Nobody But Me aliomshirikisha rapper wa Afrika Kusini, K.O nao ulitayarishwa na mtayarishaji huyo ambaye pia msanii wa kundi la Navy Kenzo. Never Ever ni miongoni mwa nyimbo zitakazowekumo kwenye album ya Vee Money, Money Mondays.
Wimbo huo unakuja kuongeza nguvu kwenye orodha ya nyimbo za Vanessa Mdee zilifanikiwa si tu Tanzania bali barani Afrika kwa ujumla. Vanessa aliyewahi kuwa mtangazaji wa kituo cha redio cha Choice FM na MTV Base, anatumbulika kama mmoja wa wasanii wa kike kutoka Afrika Mashariki waliofanikiwa zaidi.
Post a Comment