Nyimbo 5 za Diamond zilizopo stoo zitaendelea kumuweka kileleni kwa miaka 10 – asema mpiga picha wake
Diamond Platnumz ni msanii ambaye (angalau kwa sasa) haoneshi dalili za kushuka kimuziki hivi karibuni. Tunayo mifano mingi ya wasanii wa Bongo ambao waliwahi kufanya vizuri sana na baadaye kupotea kabisa kwenye ramani ya muziki.
Diamond ambaye ameachia ngoma mpya ‘Utanipenda’ wiki iliyopita ambayo imekuwa gumzo kwa watu wa kila rika, ana akiba ya hits na collabo za maana, ambazo kwa mujibu wa mpiga picha wake zinampa uhakika wa kuendelea kukaa kileleni kwa miaka mingine kumi ijayo.
Japo zipo collabo kubwa za kimataifa alizoisha fanya, ameamua kufunga mwaka kwa kuachia wimbo mwingine kabisa ambao hakuna aliyefahamu kama upo wala utafanya vizuri, hii inathibitisha silaha zilizosalia kwenye ‘benki’ yake ya nyimbo huenda yakawa ni mabomu makubwa zaidi.
Collabo zinazosubiriwa kwa hamu ni pamoja na ile ya Diamond na Ne-yo, Diamond na P-Square, Diamond na Usher na zingine
mashine 5 zilizopo store zikingoja mda mwafaka kuachiwa Ninamwona @diamondplatnumz akiendela kuwa juu kwa mika 10 #hifadhi_post_hii
— andrew kisula (@kifesiofficial) December 14, 2015
Post a Comment