Image result for tigo banner

AY na Diamond waungana kwenye remix ya Zigo

Siku hizi watu wanafanya mambo kimya kimya! Inaonekana kuwa AY amemjumuisha Diamond Platnumz kwenye remix ya hit single yake, Zigo na tayari wanafanya video nchini Afrika Kusini.
12345912_1111893075502144_366327264_n
AY na Diamond hawajasema kitu. Lakini kampuni inayotengeneza video yake imeumwaga ubuyu kwenye Instagram. Kampuni hiyo iitwayo Studio Space Pictures ya Afrika Kusini, imeweka picha hiyo juu ya wakali hao na kuandika: Earlier today with @aytanzania @ @diamondplatnumz #ZigoRemix #studiospacepictures.”
Haijulikani kama ni Diamond pekee ndiye aliyemo kwenye remix hiyo lakini kuna uwezekano mkubwa wasanii wengine wakali kuipandia beat hiyo ya Nahreel.
Hii si mara ya kwanza Diamond na AY kukutana kwenye kazi ya pamoja. Diamond amewahi kuweka ladha kwenye wimbo wa AY ‘Asante.’
CV ya Studio Space Pictures si haba. Imefanya video kali zikiwemo Phumakim ya Casper Nyovest, Sim Dope ya AKA, Marry You ya Ice Prince, Easy to Love ya Bucie, Show ya Victoria Kimani na zingine.

No comments

Powered by Blogger.