Shilole aingia studio na producer wa Yemi Alade, Selebobo
Staa wa muziki nchini, Shilole ameingia studio na producer wa hit single ya Yemi Alade (Johnny) Selebobo wa Nigeria kurekodi wimbo mpya.
Shilole ambaye yupo nchini Nigeria, ameiambia Bongo5 kuwa kila kitu kimeenda sawa na usiku wa Jumamosi waliingia studio.
“Tunaingia leo (Jumamosi) usiku studio. Nimezungumza naye nimemwonesha ngoma zangu na ametokea kupenda kazi zangu, kwahiyo kwa kifupi mashabiki wangu wategemee mambo mazuri hasa hasa kolabo,” alisema.
Shilole amesema safari yake ya Nigeria imemwezesha kukutana na wadau mbalimbali wa muziki nchini humo na kujenga uhusiano mzuri wa kazi.
Post a Comment