Mtandao 'mtakatifu' kuzinduliwa Accra-Ghana
Kundi moja la Kikristo nchini Ghana linapanga kuzindua mtandao wa kijamii ambao unaelezwa kuwa 'mtakatifu'.
Kundi hilo la Love Realm linasema mtandao huo hautakuwa na
habari, picha, sauti au hata video zenye ujumbe unaoenda kinyume na
mafundisho ya dini ya Kikristo.
Viongozi wa kundi hilo wanasema mitandao ya sasa ya kijamii imejaa picha, video na habari zenye maudhui ya utupu na ukatili.
Lakini
kundi hilo, lililoanzishwa na Dkt Yaw Ansong Jnr na Bojan Jordanovski,
limejinasibu kuwa mtandao wao ujao utawasaidia wale ambao walikuwa na
mahangaiko ya kulinda imani zao dhidi ya mitandao isiyokuwa na maadili
na mtandao huo pia utasaidia washirika wake kuungama na kutubu dhambi.
Kwa
sasa mtandao huo umekwisha waalika maelfu ya wafuatiliaji Wakristo
wafanye majaribio ya kushiriki katika tovuti hiyo katika kituo cha
Pentekoste katika mji mkuu, Accra.

Post a Comment