Mzee Majuto aingia kwenye muziki kwa namna hii
Mchekeshaji mahiri nchini, King Majuto ameamua kuingia kwenye muziki kwa namna ya kusaidia vijana wenye vipaji.
Tayari ameanza na msanii aitwaye Daddy.
Akizungumza hivi karibuni, Majuto alisema yupo tayari kuwekeza pesa yoyote ili kumsaidia kijana huyo ili afike mbali.
“Tutegemee maendeleo mazuri kwa sababu hata mimi nitamsupport sana,” alisema. “Siyo kuimba naye nyimbo tu hata kipesa nitamsaidia. Nitatoa pesa yangu na kumwambia nenda kafanye kazi mpya na ikifika wakati naweza kumpatia pesa akasomee muziki zaidi,” alisema.
Wimbo wa kwanza wa msanii huyo unaitwa ‘Baba’ ambapo Mzee Majuto anaonekana kwenye vide.
Post a Comment