Image result for tigo banner

Jux akanusha kuuza madawa ya kulevya, amzungumzia Jackie Cliff

Kufungwa kwa aliyekuwa mpenzi wake (Jackie Cliff) baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya nchini China pamoja na madai kuwa anafanya biasha ya unga, ni vitu vilivyomkosesha raha zaidi Jux.
jux-na-Jackie
Jux ambaye kwa sasa yupo nchini China kimasomo, amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM kuwa mikasa hiyo ilitikisa familia yake.
“Kitu kikubwa sana ni girlfriend wangu alipata matatizo Jackie mpaka sasa kafungwa,” alisema.
“Hii issue sawa ilikuwa inanihusu mimi kwa upande mwingine kutokana ni mtu wangu wa karibu na watu walikuwa wanajua lakini sasa kama ningekuwa sijulikani yote yasingeongelewa kwa sababu kuna vitu vilikuwa vinaongelewa ambavyo viliniaffect mimi pamoja na wazazi wangu,” aliongeza.
“Watu wengine walisema mimi nauza madawa ya kulevya wakati mimi sihusiki navyo kabisa. Lakini kama ningekuwa sijulikani na sio Jux yasingetokea ila kwa sababu ni Jux kila mtu ananijua ndio maana ikatokea hivyo lakini ni kitu ambacho kiliniumiza sana kwenye moyo wangu.”
Kwa sasa Jux na uhusiano wa kimapenzi na Vanessa Mdee.

No comments

Powered by Blogger.