Image result for tigo banner

Rafael Benitez atimuliwa Real Madrid, nafasi yake yachukuliwa na Zidane

Uongozi wa klabu ya Real Madrid hatimaye umemfukuza kocha wake Rafael Benitez ambaye amedumu kwa miezi 7 pekee.
2FCC0AEA00000578-3384137-image-m-40_1451939045866
Nafasi ya Benitez imechukuliwa na aliyekuwa mchezaji wa Ufaransa Zinedine Zidane ambaye awali alikuwa kocha wa kikosi B cha Real Madrid.
2FC5C48900000578-3383931-image-a-52_1451919569762
Hii ni kutokana na matokeo mabaya kwa timu hiyo, ambapo ilitoka sare 2-2 na Valencia, katika Mechi ya La Liga, sare ambayo imewaacha vigogo hao nafasi ya 3 wakiwa nyuma ya Atletico Madrid kwa pointi 4.
Tangu atue Madrid, Benitez amekuwa hapendwi na mashabiki wa klabu hiyo, baada ya kufungwa bao 4-0 kwenye mechi ya El Clasico mwezi Novemba na mahasimu wao Barcelona, pia kutupwa nje ya michuano ya Copa del Rey

No comments

Powered by Blogger.