Wastara afunga ndoa na mbunge Sadifa Khamis Juma (Picha)
Msanii wa filamu, Wastara Juma Alhamisi hii amefunga ndoa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama cha CCM (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Donge, Sadifa Khamis Juma.
Akizungumza na Bongo5 Ijumaa hii, Wastara amethibitisha kufunga ndoa na kueleza kwanini imekuwa ni ya kimya na ya kushtukiza.
“Wewe si umesikia? Kweli nimefunga ndoa jana,” alisema. “Ndoa ni dua tu sherehe ni maamuzi lakini cha umuhimu ni ndoa na imepita salama, tumshukuru Mungu”.
Hapo awali Wastara Juma alikuwa mke wa marehemu Juma Kilowoko aka Sujuki aliyefariki dunia January 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Post a Comment