‘Zigo Remix’ ya AY f/ Diamond imeweka rekodi hii leo duniani
Hapa AY, pale Diamond Platnumz unategemea nini kama wameshirikiana kulidondosha Zigo?
Na tena pale unapogundua kuwa watayarishaji watatu wakubwa wameshiriki kulidondosha – Nahreel aliyeupika mdundo huu, huku Hermy B na Marco Chali wakiweka mikono yao kukamilisha remix yake.
Ndio maana ndani ya saa 24, wimbo huo umesikilizwa mtandaoni kwa zaidi ya mara elfu 14! Hizo sio namba za lelemama kwa siku moja hadi kuifanya Ijumaa hii Zigo iingie kwenye Top 10 ya nyimbo zilizosikilizwa zaidi kwenye mtandao wa Audiomack.
Zigo Remix inashika namba 10 kwenye most popular songs za https://t.co/zzey1OvyUH@AyTanzania @ArthurSamTz pic.twitter.com/M90RYXgR5d
— A.K (@AbbyKirahi) January 22, 2016
Ukitaka kujua kuwa hicho sio kitu kidogo, angalia wasanii wengine waliomo kwenye top ten hiyo. Ni Wiz Khalifa, Tyga, Meek Mill, Akon na wengine
Post a Comment