Wenger: Nina wasiwasi na matokeo yetu
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger ana wasiwasi kuhusu matokeo ya timu yake na anasema wachezaji wake wanafaa kuimarika baada ya kushindwa 2-1 na klabu ya Swansea.
Baada ya mechi Wenger alisema
“Sipo kwenye mood ya kuongelea mataji usiku huu. Kwa sasa hatutakiwi kuota tena inabidi tuwe wa kweli tu.Nina wasiwasi sana kuhusu matokeo yetu, tumepoteza michezo mitatu na huu ni wakati mgumu sana kwa timu.Haya ni matokeo yanayovunja moyo sana na hali ya wachezaji ipo chini sana”
Wenger aliendelea kusema,“Tuna mechi kubwa tatu zinakuja mbele yetu na tunatakiwa kuendelea kufanya kazi ya msingi na kuonyesha ubora pia.Inabidi turudi nyuma na kufanya kama tulivyokua zamani.Ni bahati mbaya sana usiku wa leo tumetengeneza nafasi lakini tumeshindwa kumalizia”
Leicester ina pointi 57, na hivyobasi wameongeza uongozi wao katika jedwali la ligi hiyo baada ya sare ya 2-2 dhidi ya West Bromwich.
Ushindi wa Swansea unamaanisha kwamba Arsenal imepoteza mara tatu mfululizo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2010.
Post a Comment