Image result for tigo banner

Hadhi aliyopoteza Kitwanga imetokana na Bunge-Lema

Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Jonathan Lema amesema kitendo cha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kumng'oa Waziri wa Mambo ya Ndani Charles Kitwanga kunatokana na Bunge kukosa hadhi kutokana na mambo ambayo huendelea ndani ya ukumbi huo wa Bunge.


Lema ambaye ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ameyasema hayo wakati akizungumza na EATV hususu tuhuma za wabunge kunywa pombe wakati wa kazi.

''Bunge maalumu la katiba Bungeni kulikuwa na 'bar' zinauza pombe na idadi ya mawaziri na wabunge wanaokunywa pombe haijifichi ni .normal' na hii inatokana na Bunge kukosa hadhi''

''Hadhi aliyopioteza Waziri wa Mambo ya Ndani Charles Kitwanga imesababihwa na hadhi lililopoteza Bunge na wabunge na viongozi wake, siku hizi mambo yanafanyika ya ajabu polisi wanaingia ndani ya bunge wanapiga watu wanachania wanawake nguo, kanuni hazifuatwi, hivyo Kitwanga katumika tuu kwa namna ya kujiridhisha lakini kupuuzwa kwa maoni ya kambi ya upinzani ambayo yalieleza kuhusu Waziri Kitwanga kuhusika na Lugumi ndiko kulipaswa kumng'oa''-Amesema Lema.

Aidha Lema amebainisha kwamba wananchi pia wanapaswa kulumiwa kwa kitendo cha kuwachagua wabunge na kuwaacha tuu bila kuwafuatilia wanachokifanya Bungeni.

Kuhusu Bunge kutorushwa 'Live' Lema amesema kwamba inashangaza kuwaona wananchi wanakaa kimnya, viongozi wa dini na taasisi mbalimbali na kuwaachia upinzani pekee hali ambayo si nzuri kwa maendeleo ya taifa.

No comments

Powered by Blogger.