Image result for tigo banner

Mganga wa kienyeji ambaka mgonjwa wake


Mganga wa Kienyeji Hamza Saidi,(40) anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kumbaka mgonjwa aliyekwenda kutibiwa masikio kwenye ofisi ya mganga huyo.

Mganga huyo, Mkazi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji anatuhumiwa kumbaka msichana wa miaka 20, na kumsababishia maumivu makali.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa Kigoma SACP Fredinandi Mtui alisema, mganga huyo alifanya tukio hilo, Mei 15 majira ya saa tano asubuhi.

Inadaiwa kuwa msichana alifika  nyumbani kwa mganga huyo akiwa na lengo la kutibiwa masikio lakini mganga alimwambia ili dawa hiyo ifanye kazi ni lazima afanye naye mapenzi kwanza.

“Alimrubuni kuwa dawa ya sikio ili ifanye kazi inatakiwa afanye tendo la ngono na kwa ujanja huo , alimbaka msichana huyo,” alisema Kamanda.

Kamanda Mtui alisema kwa sasa mganga huyo anashilikiwa na polisi na atafikishwa mahakamani wakati wowote.

No comments

Powered by Blogger.