Image result for tigo banner

Diamond afunguka kuhusu Wema Sepetu wa sasa



Tangu waachane ni kwa muda mrefu Diamond na Wema Sepetu wamekuwa kama paka na panya.
wpid-wema-akiwa-pembeni-kumsupport-diamond1.jpg

Hali imeonekana kuwa tofauti kidogo siku za hivi karibuni baada ya Wema Sepetu kuchukua hatua na kuonekana kuanza kumsupport ex wake huyo ikiwa ni pamoja na kumuombea kura kwenye shindano la BET.
Akiongea kwenye kipindi cha Friday Night Live, kinachoruka kupitia EATV, Diamond alisema, “Kuna wakati inafika watu mnakuwa mmekua labda, mtu anaona hana sababu ya kuendelea kukuchukia au kuwa na vita na wewe, sababu mwanzo mwanzo mkiwa bado mnaenda mnaona kuna vitu mko navyo ndiyo maana kuna kuwa na chuki kubwa.”
“Lakini ikifika wakati kila mtu amesonga mbele na maisha yake, ameridhika na maisha yake anaona kwanini nimwekee vita mtu fulani hivyo nadhani labda wakati huo ndiyo huu maana mwenyewe nimeona kweli amepost BET, amepost promo ya Rich Mavoko kwangu mimi nafurahi kwa sababu naona haina faida kwa sisi wasanii kuwekeana vita,” aliongeza

No comments

Powered by Blogger.