Image result for tigo banner

Picha: Yaliyojiri kwenye bonanza la vyuo vikuu jijini Mbeya

Umoja wa vyuo vikuu jijini mbeya mwisho wa wiki iliyopita uliandaa bonanza la michezo mbali mbali iliyoshirikisha vyuo vinne, Mbeya University of Science and Technology (MUST). CBE, TIA na TEKU. Bonanza hilo lilihusisha mpira wa miguu pamoja na Netball.

Kwa upande wa Netball baadhi ya vyuo vilishindwa kuleta timu uwanjani na kupelekea kuwa na mechi moja tu kati ya MUST na TIA na ushindi ulienda kwa MUST ambao walishinda Magoli 26 kwa 24 dhidi ya wapinzani wao.

Mpira wa miguu ulishirikisha timu nne na matokeo yalikuwa kama ifuatavyo

MUST 1 -  1 TIA
TEKU 3 - 0  CBE
MUST 2 - 0 CBE
TIA 2 -  0 TEKU
TIA 0 -  1 CBE
MUST  1 - 0 TEKU

Kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo timu yenye pointi nyingi moja kwa moja inafuzu kucheza fainali. Timu ya pili na ya tatu ambazo ni TEKU na TIA zitacheza mechi ya kupata mshindi mmoja atakayeungana na MUST kucheza fainali itakayofanyika jumamosi 11 June 2016

















Timu ya Netball kutoka MUST wakiwa kwenye picha ya pamoja



CBE wakifanya mazoezi ya misuli




CBE (Walio vaa njano na nyeusi) wakiwa tayari kuvaana na TEKU
















Mashabiki kutoka TIA wakipeana mawaidha


Mashabiki kutoka MUST wakifurahia ushindi baada ya kuilaza TIA kwenye upande wa Netball

Timu ya Netball kutoka TIA



kikosi cha ushindi kutoka MUST (Waliofuzu moja kwa moja kwenda fainali)


Gwamaka mchezaji mwenye magori mengi hadi hivi sasa kutoka MUST akiwa tayari kwa mechi (3Goals)


Kikosi cha wachezaji 11 kutoka TIA




No comments

Powered by Blogger.