PICHA: Hili ndilo jina la mpira utakaotumika kwenye michuano ya EURO-2016.
Michuano ya Euro 2016 inatarajiwa kuanza rasmi leo nchini Ufaransa ambapo kutakuwa na mchezo mmoja utakaowakutanisha wenyeji Ufaransa dhidi ya Romania katika mchezo utakaopigwa kunako dimba la Stade de France majira ya saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Kama ilivyo ada katika michuano ya Ulaya, Amerika na hata ile ya dunia kwa ujumla,huwa kunakuwa na mpira maalum unaoandaliwa kwa ajili ya michunao husika ambapo katika michuano ya Euro mwaka huu, mpira utakaotumika unajulikana kwa jina la Adidas Beau Jeu,”Beau Jeu” ni jina la kifaransa likimaanisha ‘Beautiful Game’ au ‘Beautiful Play’ ambapo kwa Kiswahili maana yake ni Mchezo mzuri.
Mpira huu ulizinduliwa na Kampuni ya Adidas na kutambulishwa na mchezaji wa zamani wa Ufaransa Zinedine Zidane mwezi Novemba mwaka jana
Post a Comment