Image result for tigo banner

Polisi simamieni watu wasitucheleweshe-Rais



Rais Magufuli leo wakati wa uzinduzi wa kuboresha usalama wa raia uliofanyika katika viwanja vya Biafra amelitaka jeshi la polisi kuhakikisha linasimamia vyema na kuhakikisha hakuna mtu ambaye atachelewesha serikali katika kutimiza yale



                                Rais John Pombe Magufuli
Mambo ambayo Rais John Pombe Magufuli aliyaahidi wakati wa kampeni 2015
Rais Magufuli alisema kuwa sasa ni wakati wa kutekeleza mambo ambayo waliahidi kwa wananchi ili watu waje kumpima baada ya miaka mitano ya uongozi kama ametekeleza au laa, hivyo huu ni muda wa Serikali kufanya kazi yake pamoja na viongozi mbalimbali ambao wamepewa ridhaa na wananchi kufanya kazi zao. Hivyo asitokee mtu mmoja kumchelewesha mwingine.

"Mimi nataka nijenge reli, nataka wa kina mama waishi maisha mazuri, nataka nitatue changamoto ya maji katika mji wa Dar es salaam, nataka kujenga viwanda ili watanzania wapate ajira mbalimbali, hivyo sitegemei mtu mwingine aje kunichelewesha kutekeleza haya niliyoahidi kwa wananchi. Jeshi la Polisi simamieni jambo hili ili watu wasitucheleweshe kutekeleza yale tuliyoahidi kwa wananchi" alisema Rais Magufuli

No comments

Powered by Blogger.