Image result for tigo banner

Sijaja kupambana na Joh Makini au Fid Q- Jay Moe

Rapper Jay Moe ambaye kwa sasa ameachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la 'Pesa ya Madafu' na kuachia video ya ngoma hiyo amefunguka na kusema kuwa yeye hajarudi kwenye game ili kuja kushindana na wasanii wanaofanya vizuri sasa


bali amekuja kuleta burudani kwa mashabiki wa muziki wa Hip hop.


Akiongea kwenye kipindi cha Friday Night Live (FNL) Jay Moe amesema kuwa yeye amekuja kutoa burudani sababu amerudi vizuri kwenye game na kwenda sawa na wasanii ambao kwa sasa wanafanya poa, Jay Moe amesema kitendo cha yeye kurudi kwenye game ni kutokana na ushawishi mkubwa ambao alikuwa unaupata kwa wasanii wakubwa wa sasa ambao walikuwa wakimsihi na kumuomba arudi.


"Sijaja kupambana nao wasanii wanaofanya vizuri sasa bali nimekuja kutoa burudani kwa washabiki wetu, sababu mimi naamini washabiki wa Joh Makini ni mashabiki wa Jay Moe na mashabiki wa Fid Q ni mashabiki wa Jay Moe pia. Mimi ni msanii wa zamani ili nimerudi kivingine kama wasanii wa sasa,lakini kitu kilichonivutia mpaka kuamua kurudi kwenye game ni hawa hawa wasanii wa sasa wanaofanya vizuri sababu nipo karibu nao na ninapokutana nao wananiambia Jay Moe rudi kwenye game" alisema Jay Moe.


Mbali na hilo Jay Moe amesema amejipanga kisawasawa kwa sasa ili kuwapa burudani mashabiki zake na kusema mpaka sasa amefanyakazi na wasani wengine kama Ommy Dimpoz, Nisher ambaye ni Director na Baraka De Prince. Jay Moe amesema hatakuwa kimya kwa sababu tayari kuna kazi nyingi ameshazifanya zinasubiri muda tu wa kutoka.

No comments

Powered by Blogger.