Mauaji
ya Watanzania kwa njia ya kuchinjwa yanaendelea kushika kasi baada ya
usiku wa kuamkia jana wakazi wanane wa kitongoji cha Kibatini, kata ya
Mzizima jijini Tanga kuuawa kwa kuchinjwa shingo na watu
wasiojulikana.Watu hao ambao inadaiwa kuwa ni majambazi walivamia usiku
wa kuamkia jana kwa kuvunja milango ya nyumba tatu ambazo wakazi hao
walikuwa wamelala na kuwachinja kisha kuiba biskuti, mchele na sukari na
kutokomea navyo kusikojulikana.Wauaji hao inadaiwa wana uhusiano na
wahalifu ambao wamekuwa wakijificha ndani ya mapango ya Majimoto na
kujihusisha na matukio kadhaa cha uvamizi ili kupora vyakula na
kusababisha mauaji ya wakazi wa Jiji la Tanga, ikiwamo katika duka kuu
la Central Bakery mwishoni mwa Aprili mwaka huu.Mmoja wa shuhuda wa
mauaji hayo, Kea Leonard (70) ambaye pia ni mkazi wa Kibatini, katika
mahojiano jana alisema wanaamini kwamba chanzo cha mauaji ya wenzao ni
kulipiza kisasi.“Wiki iliyopita majira ya saa tano asubuhi hapa
tulikamata vijana saba kati ya wanane wenye umri wa kama miaka 13 ambao
walikuwa wakiranda randa hapa kitongojini ili kutafuta namna ya kuvuka
mto kwenda ng’ambo ya pili na ndipo mmoja wao alipotutoroka,” alieleza
Leonard na kuongeza:“Watoto hao tulipowaweka chini ya ulinzi na kuwahoji
tukaanza kuwatilia shaka hivyo mwenyekiti aliamua kuripoti Polisi na
ndipo hao wakawachukua kwa ajili ya mahojiano na hatukufuatilia tena
kujua kwamba waliachiwa au la kwa sababu hao watoto sio wenyeji wala
wakazi wa eneo hili.”Aliongeza kwamba wakati wahalifu hao wanavamia
nyumba ya mjumbe wa serikali ya kitongoji kabla ya kumtoa nje walisikia
mmoja wa watu hao akimhoji kuhusu mahali walipopelekwa watoto saba.
Post a Comment