Image result for tigo banner

Upinzani wazidi kumwandama Naibu Spika wa Bunge

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni leo imegoma kusoma maoni yao katika Wizara ya Fedha wakishinikiza kutokuwa na imani na Naibu Spika wa Bunge Tulia Ackson Mwansasu.

Hotuba ya upinzani katika wizara hiyo ilitakiwa kusomwa na Naibu Msemaji wa upinzani Bungeni Wizara ya fedha David Silinde ambaye amegoma kusoma maoni ya upinzani kuhusu wizara hiyo kwa kigezo cha kutokuwa na imani na Naibu Spika.

Baada ya kamati ya bajeti kusoma taarifa yake Naibu Spika alimwita msemaji wa upinzani kama ilivyo kikanuni ambapo David Silinde alitokea nje na kuomba hotuba hiyo ya upinzani iingie kwenye kumbukumbu za bunge kama ilivyo na hataisoma kwa kuwa hana imani na Naibu Spika kisha akatoka nje.

Hapo juzi Kambi ya Upinzani ikiongozwa na Kiongozi wa Kambi hiyo Freeman Mbowe walitangaza kuwa na ajenda ya kutokuwa na imani na Naibu Spika ambapo katika makubaliano yao siku ambayo Naibu huyo ataongoza kikao upinzani watatoka nje kwa kutokuwa na imani naye.

No comments

Powered by Blogger.