Image result for tigo banner

Basata wameshindwa kunipa majibu ya msingi – Roma

Msanii wa Hip Hop Bongo, Roma amesema kuwa Baraza la Sanaa la Taifa, Basata limeshindwa kumpatia majibu ya msingi juu ya sababu ya kufungiwa kwa nyimbo yake ya ‘Viva Roma Viva’.
Roma
Msanii huyo amekiambia kipindi cha ‘Hatua Tatu’ cha Times FM kuwa Basata wameshindwa kumpa sababu za msingi juu ya kufungia wimbo wake.
“Siwasemei wengine lakini mimi nilijaribu kuwauliza Basata kwanini wamefungia wimbo wangu lakini sikupewa majibu ya msingi na yenye kueleweka,” alisema Roma.
Basata waliufungia wimbo wa Roma ‘Viva Roma Viva’ mwezi October mwaka jana kwa madai kuwa wimbo huo umekiuka maadili kutokana na kuchochea ugomvi.

No comments

Powered by Blogger.