Image result for tigo banner

Dereva wa basi la City Boy ashitakiwa kwa kosa la kuua bila kukusudia na mengine 30

Aliyekuwa dereva wa moja la mabasi yaliyopata ajali ya City Boy, Jeremiah Semfungwe (34) ameshitakiwa kwa makosa 30 likiwemo la kuua bila kukusudia.



Dereva huyo alifikishwa jana kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida na kusomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi, Joyce Minde.
Jeremiah Semfungwe alisomewa mashtaka yake aliyodaiwa kutenda Julai 4 mwaka huu saa 8.15 mchana wakati akiendesha basi T 247 BCD mali ya kampuni ya City Boy kwa kuligonganisha na basi jinbgine la kampuni hiyo lenye namba za usajili wa T 331 DCE.
Naye wakili mkuu mfawidhi wa serikali, Zakaria Ndaskoi alidai kuwa siku ya tukio hilo mshitakiwa alisababisha vifo vya abiria 30 kinyume na Kifungu 195 na 198 cha Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 Toleo la Kwanza.
Hata hivyo Wakili wa mshitakiwa, Francis Kitope aliiomba mahakama impatie mteja wake dhamana kwa kuwa chini ya Kifungu 148 cha mwenendo wa makosa ya jinai, kosa hilo linadhaminika, lakini wakili Ndaskoi alipinga hoja hiyo kwa kudai kuwa kufanya hivyo kutahatarisha usalama wa mshitakiwa kwa kuwa ndugu wa marehemu na majeruhi bado wana hasira kutokana na ajali hiyo iliyotokea.
Wakili mkuu mfawidhi wa serikali, Ndaskoi aliyekuwa akisaidiana na Wakili Petrida Muta aliendelea kudai kuwa majeruhi 54 wa ajali hiyo hali zao bado ni mbaya na hatima yao haijulikani hivyo si vyema mshitakiwa kupewa dhamana.
Mshitakiwa hakutakiwa kujibu lolote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka juu ya kesi za mauji na ameswekwa rumande hadi Julai 21 kesi yake itakapotajwa tena.
Hata hivyo mshtakiwa mwingine ambaye mbaye ni dereva aliyekuwa anaendesha gari jingine la kampuni hiyo ya City Boy lililopata ajali lenye namba za usajili T 331 DCE, Boniface Mwakalukwa ametoroka.

No comments

Powered by Blogger.