Huu ndio waraka unaodaiwa kuandikwa na John Mnyika kumhusu Lowassa
Mtakumbuka
ni muda sasa sijaonekana wala kusikika katika harakati za kisiasa. Leo
nimependa kuweka bayana ili umma wa watanzania ufahamu kwani kumekuwa na
upotoshwaji mkubwa juu ya ukimya wangu.
Napenda umma wa watanzania ufahamu yafuatayo:-
1. Msimamo wangu wa kuitaka serikali
imkamate Mh Edward Lowassa, imhoji na imchukulie hatua kwa mujibu wa
sheria kutokana na ushiriki wake katika kashfa ya RICHMOND haujabadilika
kama ambavyo niliwahi kusema nikiwa mkurugenzi wa vijana wa CHADEMA tar
25 Februari 2008 na kipindi chote nikiwa Mbunge wa Ubungo.
Hivyo nategemea kuanzishwa kwa mahakama
ya mafisadi Lowassa ndiyo atakuwa wa kwa. Siwezi kusaliti msimamo wangu
bora nipoteze ubunge wangu.
2. Sikukubaliana na utaratibu uliotumika
kumpata mgombea urais ndani ya Chama changu hususani ujio wa Mh Edward
Lowassa mmoja wa watu ambao ni mizizi ya ufisadi hapa nchini. Hali hii
ilinilazimu nikae kimya kutokana na kutokuamini kilichokuwa kinatokea
hususani kwa Chama kama CHADEMA kilichojijenga na kujipatia umaarufu kwa
kuongoza mapambamo dhidi ya rushwa, ubadhirifu, ufisadi na uwajibikaji
mbovu wa serikali halafu tukasaliti msimamo wetu kwa uharaka wa kuipata
dola! Sikukubaliana na sijakubaliana hata sasa.
3. Napenda kuzungumzia utendaji wa
serikali ya Dkt Magufuli. Naomba Ifahamike nimekuwa mara zote nikisema
matatizo ya msingi ya nchi yetu hayasababishwi na mapungufu ya sheria
ila Kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na kulegea kwa misingi ya utawala
wa sheria na uwajibikaji miongoni mwa viongozi. Hivyo kwa asilimia kubwa
naona Dkt Magufuli ameweza kujibu nilichokuwa nikikilalamikia kwa muda
sasa. Haya mengine yanazungumzika.
4. Sikubaliani pia na mtazamo wa baadhi
ya viongozi wakiwemo wa Chama changu wanaotaka fedha za walipa kodi
ziendelee kuteketea kwa ufisadi na ubadhirifu huku wahusika ambao ni
wachache wakilindwa kwa kisingizio cha haki za binadamu. Kwa hili
nampongeza Mh Rais kwa msimamo na hatua anazochukua japo apanue wigo ili
watanzania maskini wanufaike na utajiri wa rasilimali walizojaliwa.
5. Vile vile naomba kuzungumzia mwenendo
wetu kambi rasmi ya upinzani bungeni au UKAWA binafsi sifurahishwi na
maagizo na maelekezo ya viongozi wetu juu ya kuingia na kutoka bungeni
kwa hoja ambazo haziwagusi wananchi moja kwa moja kiasi cha kutufanya
tushindwe kutimiza majukumu yetu kama wabunge kwa mujibu wa Ibara ya 63
(2) na (3) katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kutunga sheria,
kuisimamia serikali, kuwawakilisha wananchi na kupitisha mipango ya
maendeleo. Sifurahishwi sababu kutoka Kwetu hakuna la msingi tunalofanya
kwa ajili ya wananchi waliotutuma huko bungeni. Tusipobadilika
itatugharimu!
Mwisho nawatakia waumini wote wa kiislamu mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Imetolewa leo tar 3 Julai 2016.
John Mnyika (Mb)
Note: Mbunge John Mnyika alipohojiwa
kuhusu waraka huu, alisema kuwa siyo yeye aliyeandika na kuwa hafamu
lolote kuhusu waraka huu.
Post a Comment