‘Pale Kati Patamu’ ngoma mpya ya Nay wa mitego ni zaidi ya 'shika adabu yako'
Rapper Nay wa Mitego ameonyesha kuingiwa na wasiwasi kuhofia kufungiwa kwa wimbo wake mpya ‘Pale Kati Patamu’ ambao unatarajiwa kutoka hivi karibuni.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo wake, Saka Hela, amesema wimbo huo anaamini utachafua hali ya hewa tena kwa mashabiki kutokana na kile alichokiimba ndani ya wimbo huo.
Nay alisema kuwa akisikiliza wimbo huo yeye mwenyewe anapagawa yaani, na kuwataka mashabiki kushika hiyo tarehe kwani watathibitisha wenyewe.
“Zimebaki siku kadhaa tu, Jumatatu Tarehe 11. Nitakua naachi wimbo wangu mpya. ‘Pale kati Patamu’ hii ngoma daaah mpaka napagawa yani. Shika iyo Tarehe na siku pale kati patamu sijui wataleta zengwe na hii?” aliandika Nay Wa Mitego instagram.
Nay wa Mitego kabla ya kuachia wimbo wake wa Saka hela, alitoa wimbo uliokuwa unafahamika kama ‘Shika adabu yako’ ambao ulifungiwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).
Post a Comment