Picha za mlipuko uliotokea Saudi Arabia kwenye mji wa medina karibu na msikiti wa mtume


Mlipuko huo umetoke karibu na msikiti wa mtume uliopo kwenye mji wa Medina nchini saudi Arabia. Picha zilizoenea mtandaoni zinaonyesha moshi uliotanda juu ya anga la mji huo. Hadi hivi sasa hakuna ripoti yoyote inayoonesha nani waliohusika na shambulio hilo ikiwa ni siku kadhaa kabla ya waislamu kusherehekea sikuku ya Eid. Kuomboleza tukio hilo unaweza ungana na waombolezaji wengine duniani kwa kutumia hashtag

Zimesalia
siku kadhaa kumalizika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani lakini
katika siku za mfungo kumekuwepo na matukio ambayo kwa namna moja au
nyingine yanaishangaza dunia kutokana na maeneo ambayo yanatokea matukio
hayo kwa kuyahusisha na mwezi mtukufu.
Kama
umekuwa mtu wa kufatilia habari zinazoendelea katika mataifa mengine
utakumbuka kuwa wiki iliyopita ulitokea mlipuko katika kituo cha ndege
Istanbul, Uturuki, mlipuko uliohusishwa na IS (Islamic State) na watu
mbalimbali kujiuliza hawa IS ni Waislam au lah! maana sio jambo la
kawaida kwa Muislam kufanya tukio hilo kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Baada
ya hilo, leo jumatatu ya Julai, 7 limeripotiwa tukio lingine la kutokea
kwa mlipuko wa kujitoa muhanga katika mji wa Medina uliopo Saudi
Arabia, mji ambao unatajwa kuwa mtukufu baada ya Macca kwa watu walio na
imani ya Kiislam.
Mpaka
sasa bado hazijaripotiwa taarifa za watu kupoteza maisha lakini tukio
hilo linashangaza zaidi kutokana na sehemu ambayo mlipuko umetokea kwani
ni karibu na Msikiti wa Mtume (Prophet Mosque) sehemu ambayo inatajwa
kuzikwa Mtume Muhammad (SAW).
Katika
hili linaweza kuumiza vichwa vya Waislam wengi na watu wote duniani ni
nani anaweza kwenda kufanya tukio la kujitoa muhanga karibu na msikiti
huo kutokana na heshima uliyonayo kwa watu walio na imani ya Kiislam.

Post a Comment