Image result for tigo banner

Shilole ageuka mbogo hewani alipoulizwa maswali ya Jike Shupa na Nuh Mziwanda

Mtangazaji wa Kings FM, Divine Kweka alijikuta akitamani akate simu na aingie chini ya uvungu baada ya maswali yake kumpanikisha Shilole.
13557204_1720017804882710_1648693502_n
Mtangazaji huyo alianza vizuri mahojiano yao kwa kumuuliza kuhusu wimbo wake na Barnaba ‘Say My Name’ kabla ya mambo kugeuka alipomuuliza kuhusu Nuh Mziwanda na model wa Jike Shupa, Zuu.
“Siwezi kuzungumzia hiyo kitu sababu hainihusu,” alijibu Shishi baada ya kuulizwa anachukuliaje makavu anayopewa na ex wake.
“Sihitaji kuongelea hivyo vitu, niulize kuhusiana na muziki wangu, mambo yangu yanavyoenda, usiniulizie vitu vya watu ambao siwajui mimi,” alifoka muimbaji huyo.
Kwa upande mwingine Shilole amedai kuwa anakuja na ngoma aliyoipa jina ‘Hatutoi Kiki.’

No comments

Powered by Blogger.