Image result for tigo banner

Taarifa muhimu kuhusu Juno spacecraft iliyowasili leo July 5, 2016 Jupiter baada ya miaka mitano



'Nasa' kituo cha utafiti wa anga kutoka marekani leo July 5, 2016 wamefanikisha kwa mara ya kwanza kufikisha spacecraft inayoitwa Juno kwenye sayari ya Jupiter. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Nasa, Juno ilirushwa mnamo August 5, 2011 na kuchukua takribani miaka mitano mpaka kufika Jupiter na kuanza kuizunguka sayari hiyo kwenye mhimiri wake.
 Jupiter_diagram.svg
Launch date: August 5, 2011
Speed on orbit: 0.1056 miles/s
Max speed: 23,610 mph
Orbit height: 2,672 mi
Cost: 1.1 billion USD (2011)
Manufacturer: Lockheed Martin
 Haya ni mambo kadhaa muhimu kuhusu sayari ya Jupiter
1. Ni sayari ya 5 kwa umbali kutoka jua letu (star).
2.Ni sayari kubwa kuliko zote ktk mfumo wa jua letu.
3.Ina miezi (moons) mingi 67 kuliko sayari zote ktk mfumo wa jua letu.
4. Ni ya 4 kwa kuwa na uangavu (brightest) wa kuweza kuonekana na binadamu bila kutumia chombo cha kuonea.
5. Mwezi wa Jupiter uitwao Ganymede ni mwezi (moon) mkubwa kuliko yote ktk mfumo wa jua letu.
6.Kati ya miezi 4 (moon) mikubwa ya Jupiter, Io,Calisto,Europa na Ganymede ni ktk mwezi Europa ndiko kunakoonekana kuwa na maisha kwa mwanadamu kwani kuna maji ya kutosha na pia viumbe hai vya kwenye maji vimegundulika kuwepo kama samaki.
7. Jupiter kwa ukubwa wake ilitosha kuwa jua (star) lakini tendo la kuwa linalizunguuka jua letu ndio limefanya likose sifa ya kuitwa jua(star)
8. Ukiwa Jupiter uzito wako ni mara 2 na nusu ya duniani,hii inamaanisha kuwa, kwa mfano kuku na kanga wetu hawawezi kuruka wakiwa Jupiter.
9. Siku (day) ndani ya Jjupiter ni fupi mno ndani ya saa 9 siku imekwisha.

Tazama video team nzima ya Nasa wakipongezana baada ya mafanikio waliyoyafikia

No comments

Powered by Blogger.