Mshambuliaji wa England na Tottenham, Harry Kane atasaini mkataba
mpya kusalia White Hart Lane wenye thamani ya pauni milioni 5 kwa mwaka
wiki hii (Independent).
Jose Mourinho ana uhakika wa kumshawishi kiungo kutoka Ufaransa Paul
Pogba, 23, kurejea tena Manchester United miaka minne baada ya kuondoka
na kwenda Juventus (Daily Mail).
Manchester United wapo tayari ‘kuvunja benki’ ili kumsajili Pogba, huku dau likidhaniwa kufika hadi pauni milioni 100 (Telegraph).
Kiungo wa Paris St-Germain, Blaise
Matuidi, 29, amepewa ruhusa ya kuondoka katika kambi ya Euro 2016 ya
Ufaransa na kwenda England kwa ajili ya mazungumzo ya kuhamia Manchester
United (Goal).
Manchester United na Liverpool wote wanataka kumsajili kiungo wa Porto Ruben Neves, 19 (Sun).
Manchester City wanakaribia
kukamilisha usajili mwingine unaodhaniwa kuwa wa pauni milioni 40
kumchukua winga wa Schalke, Leroy Sane, 20 (Manchester Evening News).
Tottenham hatimaye wanakaribia
kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa AZ Alkmaar, Vincent Janssen, 21,
wiki hii na pia wanataka kumsajili mshambuliaji wa Roma, Antonio
Sababria, 20 na Lucas Alario, 20 kutoka River Plate (Daily Mirror).
Arsenal wako tayari kumpa Alvaro Morata, 23, mshahara wa pauni 144,000 kwa wiki kumshawishi kuhamia Emirates (Don Balon).
Crystal Palace wameongeza dau lao
kufikia pauni milioni 31.5 kumtaka mshambuliaji wa Liverpool Christian
Benteke, 25, baada ya dau la pauni milioni 25 kukataliwa (Sun).
Crystal Palace wanakamilisha uhamisho wa beki wa West Ham James Tomkins, 27 (Evening Standard).
Chelsea wanafikiria kutoa pauni
milioni 12 kumchukua mshambuliaji wa Southampton Graziano Pelle, 30,
iwapo watashindwa kumpata Morata kutoka Real Madrid (Evening Standard).
Kiungo wa Liverpool Lucas Leiva, 29, yuko tayari kuhamia Besitkas ya Uturuki (Fanatik).
Fernabahce wanataka kumsajili mshambuliaji wa Newcastle Siem de Jong, 27 (Haberturk).
West Ham na Crystal Palace ni
miongoni mwa timu za EPL ambazo Robin van Persie, 32, ameruhusiwa kwenda
na klabu yake ya Fernabahce (Daily Mail).
Mshambuliaji wa zamani wa Aston
Villa Charles N’Zogbia, 29, anajaribu kufufua mpira wake kwa kufanya
mazoezi na Sunderland (Birmingham Mail). Tetesi nyingine kesho
tukijaaliwa.
Post a Comment