Image result for tigo banner

Shetta asema ushindani uliopo kwenye muziki umemfanya aogope kutoa ngoma mbaya

Hit maker wa wimbo ‘Namjua’ Shetta amefunguka kwa kusema kuwa yeye ni mmoja kati ya wasanii ambao hawajawai kutoa ngoma mbaya katika maisha yake ya muziki.
prima
Akiongea na Bongo5 Jumapili hii, Shetta amesema biashara ya muziki imefanya afanye muziki wa kushindana kila siku ndio maana kila akitoa ngoma anahakikisha ni kali.
“Shetta sasa hivi ni mfanyabiashara, muziki wangu ni bidhaa adimu ndio maana mimi sijawai kutoa ngoma alafu isifanye vizuri, ni hit baada ya hit na ndo maisha yangu kwa sasa, na nitaendelea kufanya hivyo,” alisema Shetta.
Rapper huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kusubiria surprise ya wimbo wake mpya baada ya ‘Namjua’ kufanya viruri.

No comments

Powered by Blogger.