Image result for tigo banner

Wanachama wa Yanga waamua yafatayo kuhusu Manji


Yanga-maadhimio
 Maamuzi yalifikiwa na wanachama wa Yanga Kikao cha Leo baada ya Manji Kutangaza kuachia uwenyekiti wa klabu
1. Kupokea kwa masikitiko kusudio la kujitoa uenyekiti-Mwenyekiti wetu.
2. Kulaani taarifa ya anayejiita Katibu wa wazee-Mzee Akilimali.
3. Kumuomba mdhamini mzee Katundu kumuondoa mzee Akilimali kwenye nafasi ya Katibu wa wazee.
4. Kuwaomba wanachama watulie na kuuachia uongozi ufanyie kazi suala hili.
5. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam tunamheshimu lakini kwenye tamasha la Simba alijionesha yeye ni Simba. Tunamuomba atuachie Yanga yetu hatutaki aizungumzie Yanga.
6. Tunamlaani mtangazaji wa Magic FM Cyprian Musiba asitumie chombo hicho kumtukana Mwenyekiti wetu.
7. Tunaomba kamati ya utendaji imuite mzee Akilimali imhoji na asimamishwe, wanachama wanamtuhumu kuwa yeye ni Simba.
8. Hitimisho matawi yote na wanachama wote wanaendelea kumtambua Manji.

No comments

Powered by Blogger.