Image result for tigo banner

Nilikua nikilala studio kabla sijahamia kwa shilole - Nuh Mziwanda

Nuh Mziwanda alikuwa akiishi kwenye studio ya muziki kabla ya kuhamia kwa mpenzi wake Shilole.
11856765_513869878768881_1503377325_n
Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Hatua Tatu cha Times FM kuwa awali hakuwa na makazi maalum mpaka alipohamia kwa Shishi.
“Nilikuwa nalala studio, nashinda studio tu. Zamani makazi yangu yalikuwa studio, nilikuwa producer studio moja hivi Ilala, so siku niliyoenda kwa Shilole nilienda na begi tu,” alisema.
Kwa upande mwingine Nuh alidai kuwa maisha ya vituko wanayoishi na mpenzi wake wameyachagua.

No comments

Powered by Blogger.