Image result for tigo banner

Weusi washoot video 2 mpya na Justin Campos, Afrika Kusini. Moja ni ya Joh Makini na nyingine ya G-Nako

Joh makini na G-Nako ambao wako nchini Afrika Kusini, wamekamilisha kazi iliyowapeleka huko ambayo ni kushoot video mbili.
11821119_1609709415949187_1581297285_n
Video ya kwanza ni ya collabo ya Joh Makini na rapper wa Afrika Kusini, AKA ambayo (audio) ilirekodiwa May mwaka huu, rapper huyo alipokuja Tanzania kwenye Zari All White Party. Wimbo huo unaitwa ‘Don’t’ Bother’.
Video ya pili ni ya G-Nako ya wimbo unaoitwa ‘Original’. Video zote zimeongozwa na director anayekuja juu sana kwa sasa Justin Campos ambaye alifanya video ya Joh Makini ‘Nusu Nusu’. 
"PROJECT KILA BAADA YA PROJECT KWA SABABU NI PROJECT 2VIDEOS DONE JOH MAKIN FT A.K.A (DONT BOTHER) ,G.NAKO…..ORIGINAL DIRECTED BY JUSTIN CAMPOS PRODUCED BY NAHREEL (THE INDUSTRY) WEUSI KAMPUNI INTERNATIONAL VIBE"
ameandika Nikki Wa Pili Instagram.



Nikki Wa Pili ameiambia Bongo5 kuwa yeye anatarajia kufanya video na Justin Campos mwishoni mwa mwaka huu.
Hii ni hatua nyingine kwa Weusi kuendelea kujitangaza zaidi kimataifa. Video ya ‘Nusu Nusu’ licha ya kuonekana kwenye vituo vya kimataifa kama MTV Base na Trace Urban lakini pia ilifanikiwa kushika namba 1 kupitia chati za MTV Base.

No comments

Powered by Blogger.