Kilichomkuta Cannavaro baada ya kuonyesha kum-support Magufuli
Headlines za uchaguzi mkuu 2015 bado
zinazidi kuchukua nafasi, tumekuwa tukiona watu maarufu kama wasanii wa
filamu na Bongofleva wakionyesha hisia zao kwa wagombea wawapendao. Ila
kwa wachezaji mpira wa miguu ni tofauti kidogo kulingana na sheria za
vilabu vyao pamoja na mikataba yao.
Baada ya kuonekana kwa picha ya nahodha wa klabu ya Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Nadir Haroub Cannavaro
akimsuport moja kati ya wagombea Urais wa mwaka 2015, kumekuwa na stori
nyingi sana kuhusiana na sheria ya wachezaji kuonesha hisia zao kwa
vyama wavipendavyo hususani wakiwa wamevaa jezi za vilabu vyao.
Katibu mkuu wa Yanga Dk Jonas Tiboroha
Ripota wa millardayo.com alipata nafasi ya kufanya exclusive interview na katibu mkuu wa Yanga Dk Jonas Tiboroha na kuzungumzia kuhusiana na Cannavaro kuvaa jezi za Yanga na kupiga picha akionyesha hisia zake kwa mgombea huyo.
“Mimi
nafikiri Cannavaro angekwenda akiwa amevaa nguo zake za kawaida na
kuonyesha kumsuport Magufuli au mwingine isingekuwa na tatizo. Sisi
tunachozungumzia ni yeye kuvaa jezi ya klabu na yenye nembo ya mdhamini
wetu halafu unaonyesha kushabikia siasa, Cannavaro amekosea hivyo kama
klabu tumekaa chini na tutaangalia hatua za kinidhamu zipi
zichukuliwe” Cannavaro
Post a Comment