Image result for tigo banner

Man United yapata pigo baada ya beki wake Luke Shaw kuvunjika mguu

Manchester United imepata pigo baada ya beki wake wa kushoto, Luke Shaw kuvunjika mguu. Kutokana na majeraha hayo, mchezaji huyo atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi sita.
2C5A162700000578-3235800-Manchester_United_defender_Luke_Shaw_holds_his_leg_after_sufferi-m-48_1442347227257
Luke aliumua kwenye mchezo wa jana wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya wenyeji PSV nchini Uholanzi. Katika mchezo huo United ililala 2-1. Shaw alimwaga machozi wakati anatolewa nje kutokana na uchungu wa maumivu makali.
2C5A819E00000578-3235831-image-a-57_1442347972279
Alipatiwa huduma ya kwanza hapo hapo uwanjani na aliwekewa hewa ya ziada mjini Eindhoven kabla ya kukimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi.
Luke atarejeshwa Manchester ambako anatarajiwa kufanyiwa upasuaji.

No comments

Powered by Blogger.