Image result for tigo banner

Ne-Yo kaimba Kiswahili kwenye wimbo alioshirikishwa na Diamond – Sheddy Clever

Producer Sheddy Clever aliyehusika na upishi wa collabo kubwa ya kimataifa ya staa wa Tanzania, Diamond Platnumz na mwimbaji wa R&B kutoka Marekani, Ne-Yo amedokeza kidogo kuhusu wimbo huo.
sheddy neyo
Mtayarishaji huyo wa Burn Records amesema kuwa Ne-Yo aliimba baadhi ya maneno ya Kiswahili katika verse yake.
“Ne-Yo kaimba Kiswahili katika single hiyo, Diamond alimuimbisha Kiswahili siwezi kusema ni maneno gani ya kiswahili bali watu wakae mkao wa kula” Sheddy aliiambia Millardayo.com.
Hii si mara ya kwanza kwa Diamond kuwaimbisha Kiswahili wasanii wa kimataifa anaofanya nao collabo, alifanya hivyo pia kwenye remix ya Number One aliyomshirikisha Davido, ambaye naye aliimba maneno machache ya Kiswahili

No comments

Powered by Blogger.