Image result for tigo banner

Siri kuhusu WYNE ROONEY


Kitu ambacho kilikuwa hakijulikani kwa mda mrefu ni kwamba mchezaji wa Manchester United Wyne Rooney alitumiwa ofa ya kusajiliwa na United mara mbili na kiukataa kipindi yupo Everton. Taarifa hizo zimetolewa na alie kuwa kocha wa zamani wa klabu hiyo Sir. Alex Ferguson. Kocha huyo amesema klabu ilitaka kumsajili mchezaji huyo akiwa na miaka 14 akiwa kwenye academy ya Everton ili ajiunge na Academy ya Manchester United lakini aliweza kuikataa ofa hiyo.
Ferguson amesema Rooney alikuwa anaipenda na shabiki mkubwa wa Everton kitu hicho kilimfanya mchezaji huyo kutokubali kujiunga na klabu ya Manchester United. Baada ya miaka miwili Rooney akiwa na miaka 16 alitumiwa tena dau la kuhamia United lakini bado liligonga mwamba.
 
Sasa hivi akiwa kapteini wa klabu ya Manchester United ameweza kufanya mambo makubwa sana ikiwa ni kuchukua vikombe vingi.
 



No comments

Powered by Blogger.