Image result for tigo banner

Blatter na Platini wakalia kuti kavu, kamati yataka wawajibishwe

Kamati ya maadili katika shirikisho la soka duniani FIFA imependekeza Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA, Sepp Blatter asimamishwe kazi kwa siku 90, yeye pamoja na Rais wa UEFA Michel Platini ili kupisha uchunguzi wa ubadhilifu wa fedha wa wakati wa kipindi cha utawala wa Blatter.
2D2D7D2200000578-3264067-image-a-159_1444250273418
Wanachama wa kamati hiyo walikutana wiki hii baada ya Jaji mkuu nchini Uswizi kufungua mashtaka ya uhalifu dhidi ya Blatter mwezi uliopita.
Blatter anatuhumiwa kwa kutia saini kandarasi zisizo na manufaa yoyote kwa FIFA mbali na kufanya ‘malipo’ kwa rais wa shirikisho la UEFA Michel Platini.
Blatter amekuwa rais wa FIFA tangu mwaka 1998 na Platini ambaye anataka kumrithi amekana madai yoyote ya kufanya uovu.
Hakuna uamuzi ulioafikiwa kuhusu kumchukulia hatua yoyote Platini.

No comments

Powered by Blogger.