Image result for tigo banner

Jose Mourinho ashtakiwa kwa utovu wa nidhamu na FA

Chama cha soka nchini Uingereza FA kimemshtaki meneja wa Chelsea Jose Mourinho kutokana na utovu wa nidhamu baada ya matamshi yake juu ya maafisa wa soka wa FA kuhusika kwenye kichapo cha goli 3-1 dhidi ya Southampton siku ya Jumamosi.
 jozee2
FA imedai kuwa maoni hayo yalikuwa yakijaribu kuashiria kwamba kulikua na upendeleo kwa upande fulani.
Mourinho alimlalamikia mwamuzi Robert Madley kwa kuwakatalia Chelsea penalti siku ya Jumamosi na kusema kuwa maofisa wa mchezo walikuwa hawataki timu yake ishinde mchezo huo.
Mreno huyo mwenye miaka 52 amepewa hadi Oktoba 8 kujibu tuhuma hizo.
Kwa kufungwa na Southampton ina maana kuwa Chelsea imepoteza michezo minne kati ya minane ya ufunguzi wa ligi msimu huu huku wakiwa alama 10 nyuma ya vinara Manchester City na alama 4 juu ya mstari wa kushuka daraja

No comments

Powered by Blogger.